VIONGOZI KAUNTI YA UASINGISHU WAHAKIKISHIA WAKAAZI WA ENEO HILO USALAMA WAKATI WA UCHAGUZI.


Gavana Jackson Mandago ametoa hakikisjo kwa wenyeji kwamba amani itaendelea kudumu kabla wakati na hata baada ya uchaguzi wa agosti tisa na hivyo akawataka kutoishi na wasiwasi
Akizungumza katika eneo la Kimuri aidha amewataka wanasiasa kuuza sera zao kwa wananchi bila ya kutoa matamshi ambayo yanaweza kuwatia wenyeji hofu huku akiongeza kwamba kila mwanasiasa yuko huru kujitaftia kura katika kaunti hiyo kwa njia ya amani.