WANAWAKE TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA SEKTA YA JUA KALI.


Kutokana na mchango wa sekta ya jua kali kwa uchumi wa taifa ambayo ni asilimia ishirini na tano wakenya wa jinsia ya kike wameshauriwa kujiunga na sekta hiyo ili kunufaika na fedha na mashine za kufanyia kazi kutoka kwa serkali
Wakati wa kikao na wanahabari baada ya shirika la lower jua kali mjini kitale kupokezwa mashine za aina mbalimbali, mkurugenzi wa mamlaka ya biashara ndogo karani njeru amesema serikali imetenga shilingi takriban bilioni moja kuwekeza kwenye sekta hiyo kote nchini.
Kwa upande wake afisa anayesimamia uzalishaji na kilimo biashara katika shirika hilo Tabitha Gicheru amewataja akina mama kuwa nguzo kuu katika ukuzaji wa uchumi na kwamba mikakati mwafaka imewekwa kuhakikisha wanajiunga na sekta hiyo.
Mwenyekiti wa kitale lower juakali association peter sifuna amesema kuwa mashine hiyo itarahisisha pakubwa kazi yao kwani wamekuwa wakipitia changamoto nyingi katika sekta hiyo.