KIWANGO CHA SAMAKI TURKWEL CHAONGEZEKA
Kiwango cha samaki katika bwawa la Turkwel katika kaunti hii ya Pokot magharibi kimeongezeka hali ambayo imepelekea kuimarika biashara ya samaki eneo hili.
Mwenyekiti wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio valley KVDA Mark Chesergon amesema kuwa hali hii imetokana na hatua ya mamlaka hiyo kuweka samaki wapya wadogo wa kufugwa katika bwawa hilo miezi sita iliyopita katika juhudi za kuimarisha biashara hiyo kwa wakazi.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na afisa katika huduma ya uvuvi Kenya fishery service eneo la kaskazini mwa bonde la ufa Ann Naporom ambaye aidha amesema uzani wa samaki hao umeimarika ikilinganishwa na samaki wa awali.
Wafanyibiashara wa eneo hilo wameelezea kunufaika pakubwa na biashara hiyo ya samaki