MIITO YA AMANI MSIMU WA UCHAGUZI YAENDELEA KUTOLEWA.
Mwaniaji wa kiti cha Mwakilishi wadi ya Mnagei kaunti hii ya Pokot magharibi kupitia chama cha ODM Richard Mwareng’ ameahidi kuimarisha maisha ya vijana iwapo atachaguliwa kuongoza wadi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Mwareng’ amesema atafanya kila awezalo kubuni nafasi mbalimbali za ajira ili kupunguza idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na ajira.
Aidha Mwareng amewasihi vijana katika kaunti hii kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua vurugu katika mikutano ya wapinzani wao kwa manufaa yao ya binafsi na badala yake kujihusisha na maswala ambayo yatawanufaisha maishani.