MWANAKANDARASI ANAYE WEKA LAMI BARABARA YA LESOS KOLONGOLO ASHUTUMIWA NA WAKAAZI KWA KAZI DUNI
Wakaazi wa eneobunge la kwanza wamepaza sauti zao kulalamikia hatua ya Mwanakandarasi kutia Lami Barabara ya Lesos Namanjalala Kolongolo ambayo haiwezi kutumika na malori yanayobeba mizigo yenye uzani unazidi tani kumi
Wakaazi hao akiwemo Kennedy Serem na FrAncis Letei wamesema Barabara hiyo inayojengwa kwa kima cha shilingi bilioni mbili nukta tatu imekuwa ikiharibiwa na malori ambayo husambaza mazao ya shambani na malori ya kubeba changarawe kutoka kanyarkwat
Hata hivyo Mkurugenzi wa utekeleza wa miradi ya serkali katika ofisi ya rais Tuitha Richard amesema ni hatia kwa madereva kubeba mizigo kupita kiasi na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka hilo