MAAFISA KATIKA IDARA YA USALAMA WALAUMIWA KWA KUINGILIA SIASA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Mgombea ugavana katika kaunti hii ya Pokot magharibi kupitia chama cha UDA Simon Kachapin amewalaumu maafisa katika idara ya usalama nchini kufuatia kukithiri utovu wa usalama hasa katika eneo la bonde la Kerio.
Akizungumza na kituo hiki Kachapin ambaye ni gavana wa kwanza wa kaunti hii amesema kuwa inasikitisha kwamba licha ya serikali kutengea idara ya usalama mgao mkubwa zaidi maafisa katika idara hiyo wameendelea kuzembea katika kutekeleza majukumu yao.
Wakati uo huo Kachapin amemshutumu mshirikishi wa serikali eneo la bonde la ufa Mohamed Maalim kwa madai ya kuwashurutisha machifu kupigia kura mrengo wa azimio la umoja katika ziara yake kaunti hii badala ya kuweka mikakati ya kuimarisha usalama eneo hili.
Kachapin amesema si demokrasia kwa yeyote kushurutishwa kumpigia kura mgombea fulani akisisitiza kuwa maafisa wa serikali hawapasi kuonyesha miegemeo ya kisiasa.