SHULE YA UPILI YA WAVULANA YA ORTUM YANGAA KATIKA MTIHANI WA KITAIFA
Shule ya upili ya Ortum katika kaunti hii ya Pokot magharibi ni miongoni mwa shule ambazo zilikuwa zikifahamika zaidi kwa visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi ikiripoti visa vya kuteketezwa majengo ya shule kila mara na kupelekea kudorora matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Hata hivyo kulingana na naibu mkuu wa shule hiyo Nelson Nyang’aita mikakati ambayo iliwekwa na uongozi wa shule hiyo katika kukabili tatizo hilo imesaidia pakubwa kurejesha nidhamu miongoni mwa wanafunzi hali ambayo imeanza kurejesha hadhi yake.
Aidha kulingana na Nyag’aita mikakati hiyo ilisaidia shule hiyo kufanya vyema katika mtihani wa kitaifa KCSE mwaka 2021 hasa baada ya shule hiyo kurekodi alama 6.134 ikilinganishwa na miaka ya awali, ishara kuwa shule hiyo inarejesha hadhi yake.