WAKAZI TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUWACHAGUA VIONGOZI WATAKAOIMARISHA MAISHA YAO.
Ipo haja ya kuwachagua viongozi bora watakaojali maslahi ya wapiga kura ikiwemo usalama mbali na maendeleo mashinani.
Akiongea katika Wadi ya Tuwani Kaunti ya Trans Nzoia mwanasiasa Mathew Njoroge amewarai wakazi katika Wadi hiyo kuwachagua viongozi walio na maono pasipo kuzingatia vyama akisema kina Mama na vijana wanahitaji kupigwa jeki ili kuinuka kiuchumi.
Ni kauli iliyoungwa mkono na mwanaharakati wa amani Yonah Chebus ambaye amewashauri Wakenya hasa wakazi wa Kaunti ya Trans Nzoia kuepuka swala la kuwachagua viongozi kwa misingi ya kikabila au vyama kwa kile anasema suala hilo limeathiri pakubwa maendeleo.
Aidha amewataka wapiga kura kufanya uamuzi wao wenyewe bila kushurutishwa na mrengo fulani wa kisiasa nchini.