MCHUJO WA UDA WAZIDISHA MACHOZI ELGEYO MARAKWET.
Aliyekuwa inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett amejitokeza na kupinga matokeo ya mchujo wa chama cha UDA katika kinyang’anyiro cha ugavana kaunti ya Elgeyo marakwet akidai matokeo yalikarabatiwa kumpendelea naibu gavana Wesley Rotich.
Akiongea mjini Eldoret kaunti ya Uasin gishu, hata hivyo Boinnet ametangaza kuwa hatawania wadhifa huo kama mgombeaji huru wala kukata rufaa kwa bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama hicho.
Boinnet ameongeza kuwa ingawa Rotich alitangazwa mshindi kwa zaidi ya kura 42,000, matokeo yaliyojumlishwa na timu yake yalionyesha kuwa takwimu zilibadilishwa kwa kiasi kikubwa huku akizoa takriban kura 32,000 na kuwa wa pili
Boinett aidha amewalaumu watu wanne anaodai walivuruga matokeo ya uchaguzi huo japo ni marafiki wake na watu ambao walizungumza baada ya shughuli hiyo ya mchujo.