VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WALALAMIKIA ATHARI ZA UKAME.


Mwakilishi wadi ya masol katika kaunti hii ya Pokot magharibi Ariong’o Loporna amelalamikia ongezeko la hali ya ukame eneo hilo.
Akizungumza na kituo hiki Loporna amesema kuwa wakazi wengi wa eneo hilo wameathirika pakubwa kutokana ukame ambapo idadi kubwa ya mifugo wameangamia licha ya kuwa ndilo tegemeo kubwa la uchumi wa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi.
Aidha Loporna amedai hali ya ukame imepelekea kukithiri visa vya wizi wa mifugo kutokana ukosefu wa chakula miongoni mwa wakazi wengi akitaka hatua za haraka kuchukuliwa kuokoa hali.
Loporna sasa anatoa wito kwa serikali kupitia idara ya majanga kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya unyunyiziaji maji mashamba.