CHAMA CHA UDA CHATAKIWA KUZINGATIA UWAZI KATIKA MCHUJO ELGEYO MARAKWET.


Wawaniaji wa viti mbalimbali katika kaunti ya Elgeyo marakwet kupitia chama cha UDA wamewataka wasimamizi wa uteuzi ulioratibiwa kufanyika siku ya alhamisi wiki hii kuhakikisha panakuwa na uwazi katika shughuli hiyo nzima.
Wakiongozwa na mwaniaji wa kiti cha ubunge wa marakwet magharibi Timothy kipchumba wamewaonya waandalizi dhidi ya kukiuka sheria kwenye uteuzi huo wakisema kuwa watakabiliwa kisheria.
Kipchumba hata hivyo ameeleza matumaini na chama cha UDA kuwa kitaweza kuendeleza shughuli hiyo bila changamoto zozote akiwataka wawaniaji wengine kutokuwa na wasiwasi.