TOFAUTI ZAENDELEA KUSHUHUDIWA BAINA YA GAVANA NA NAIBU GAVANA POKOT MAGHARIBI.
Naibu gavana kaunti hii ya Pokot magharibi Nicholas Atudonyang amemsuta vikali gavana John Lonyangapuo kwa kile amedai kuendeleza wizi wa fedha za umma huku wakazi wa kaunti hii wakihangaika kwa kukosa huduma muhimu.
Akizungumza alipokutana na baadhi ya wanachama wa chama cha KANU kaunti hii Atudonyang amemsuta Lonyangapuo kwa kile amedai kufuja fedha zilizonuiwa kuboresha sekta ya afya kaunti hii pamoja na elimu.
Atudonyang amewataka wakazi wa kaunti hii kuhakikisha wanafanya uamuzi wa busara katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti kwa kuwaondoa viongozi wasiowajibika, huku akiahidi kuhakikisha ufisadi unakabiliwa kaunti hii iwapo atachaguliwa gavana katika uchaguzi mkuu ujao
Wakati uo huo Atudonyang ameahidi kuimarisha zaidi sekta ya afya hasa hospitali ya Kapenguria kwa kuhakikisha huduma za matibabu zinaimarishwa katika hospitali hiyo kwa manufaa ya wananchi.