VIONGOZI WA AZIMIO LA UMOJA WAELEZEA IMANI YA KUTWAA UONGOZI WA TAIFA.
Seneta wakaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amesema kuwa mrengo wa azimio la umoja uko katika nafasi bora ya kuongoza taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao wa mwezi agosti.
Poghisio amesema kuwa hatua ya kinara wa chama cha KANU Gideon Moi, mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka na Martha Karua wa chama cha Nark Kenya kujiunga na muungano huo inaipa azimio la umoja nguvu zaidi za kutwaa uongozi wa taifa.
Wakati uo huo Poghisio amemtetea kinara wa chama cha Nark Kenya Martha Karua kutokana na madai kuwa hajaongeza uzito wowote kwenye mrengo huo akisema kuwa wanaoeneza madai hayo hawana ufahamu kuhusu umaarufu wa kiongozi huyo.