GAVANA LONYANGAPUO AWAHIMIZA WANASIASA KUKOMA KUINGIZA SIASA KATIKA MASWALA YA AFYA

Gavana wa kaunti ya pokot magharibi john lonyangapuo ameongoza zoezi la uzinduzi wa dawa zitakazotumiwa katika vituo vyote vya afya kwenye kaunti hii
Katika mazungumzo ya kipekee na idhaa hii gavana lonyangapuo amekariri kujitolea kwa utawala wake kukidhi mahitaji ya wenyeji ,akipuzilia mbali madai ya uhaba wa dawa katika hospitali kaunti nzima.
Amewasuta wanasiasa wanaoendelea kupaka tope utawala wake akisema ni muhimu kwao kuuza sera zao kwa wananchi badala ya kumzungumzia vibaya kila mara
Aidha lonyangapuo amesema ataendelea kuipa kipau mbele maswala yanayowafaidi wananchi moja kwa moja ikiwamo elimu akisema watu zaidi ya miambili watafuzu juma lijalo baada ya kupata mafunzo kuhusu ushonaji wanguo