MAJAMBAZI WAWAJEUHI MAAFISA WA POLISI NA MENEJA WA BENKI YA COOPERATIVE MJINI KIMILILI KAUNTI YA TRANSNZOIA NA KUTOWEKA NA MILIONI 25.
Maafisa wa polisi wawili ambao walikuwa wakisafirisha fedha za wakulima wa kahawa kutoka benki ya cooperative mjini Bungoma hadi chama cha ushirika cha Kimilili mjini, pamoja na meneja wa chama hicho cha ushirika cha Kimilili wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na majambazi punde tu walipofikisha fedha hizo.
OCPD wa wa kaunti ndogo ya Kimilili Mwita marwa amesema majambazi hao waliwavamia maafisa hao muda mfupi tu baada ya kuwasili katika eneo la chama cha ushirika na kutoweka na shilingi milioni 25 wakitumia gari aina ya salun.
Wakulima waliokuwa sehemu ya tukio wamesema kuwa wahalifu hao walikuwa wawili na walikuwa wamejihani kwa bunduki wakivizia usafirishaji wa pesa hizo.
Mbunge wa Kimilili Didmus Baraza amelalamikia ukosefu wa usalama eneo hilo huku akitaka wizara husika kuingilia kati swala la usalama.