WALIMU WAKUU WAMEONYWA DHIDI YA KUJIHUSISHA NA MASWALA YA WIZI MITIHANI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Maandalizi yote kwa ajili ya mitihani ya kitaifa mwaka huu kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nane KCPE na wale wa kidato cha nne KCSE ambayo inaanza mwezi huu wa machi yamekamilika.
Akizungumza katika hafla ya maombi kwa ajili ya mitihani ya kitaifa katika shule ya upili ya Chewoyet, mkurugenzi wa elimu kaunti ndogo ya Kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Charles Manyara aidha ameonya dhidi ya jaribio lolote la udanganyifu katika mitihani hiyo huku pia akiwataka wazazi kuwapa muda bora watoto wao kwa ajili ya mitihani hiyo.
Manyara amesema kuwa kinyume na miaka ya awali mwaka huu visa vya watahiniwa ambao watafanya mitihani wakiwa wajawazito vimepungua mno huku akiwapongeza wadau mbali mbali wakiwemo wazazi, walimu pamoja na machifu kwa kuchangia kupungua visa hivi.
Kwa upande wao wazazi wakiongozwa na mwenyekiti wa wazazi wa shule hiyo Robert Otsiula wameridhishwa na maandalizi ya mitihani hiyo wakielezea matumaini ya matokeo bora licha ya chanagamoto ya janga la corona.