UONGOZI WA GAVANA LONYANGAPUO WAKOSOLEWA NA ALIYEKUWA GAVANA WA KWANZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI



Uongozi wa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo umeendelea kutiwa kwenye mizani na wapinzani wake katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Aliyekuwa gavana wa kaunti hii Simon Kachapin ameendelea kutetea uongozi wake aliohudumu kama gavana wa kwanza wa kaunti hii akisema kuwa alitekeleza mengi ikilinganishwa na gavana Lonyangapuo licha ya kutengewa bajeti ya chini zaidi kinyume na ya sasa.
Aidha Kachapin ambaye ametangaza nia ya kuwania tena kiti cha ugavana kaunti hii amemshutumu gavana Lonyangapuo kwa kile amedai kuwa alifanyia marekebisho bajeti katika bunge la kaunti hii kwa manufaa yake akisema kuwa hatua hiyo ni ya uhalifu na tamaa ya uongozi.
Wakati uo huo Kachapin ameendelea kukosoa hatua ya gavana Lonyangapuo kuzindua chama kipya cha kisiasa cha KUP akidai kuwa hakitafika popote ikizingatiwa baadhi ya wanachama wameanza kughura chama hicho.