KNUT CHATISHIA KUSITISHA SHUGHULI ZA ELIMU BONDE LA KERIO.
Viongozi wa chama cha kitaifa cha walimu KNUT na chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET kwenye eno la kaskazini mwa bonde la ufa , wametishia kuwashauri wanachama wao kwenye maeneo ambayo yanashuhudia ukosefu wa usalama kusitisha shughuli za masomo.
Wakitoa taarifa kwenye vyombo vya habari mjini Eldoret, viongozi wao wameilaumu serikali kwa kukosa kuwahakikishia walimu na wanafunzi kwenye bonde la kerio usalama.
Katibu wa KUPPET kwenye kaunti ya Baringo Zachary Nyoboi ameilaumu serikali kwa kutochukua hatua zifaazo kudumisha usalama kwenye maeneo hayo na kukosa kuwashughulikia wenzao walioathirika na ukosefu wa usalama.
Aidha wameelezea wasiwasi kwamba huenda wanafunzi kwenye shule zilizo kwenye bonde la kerio na kwingineko kunakoshuhudiwa mashambulizi ya mara kwa mara wakafeli mtihani wao , huku akitaka serikali kuwatuma maafisa wa usalama zaidi kwenye maeneo hayo wakati wa mitihani .
Paul Biwott ni katibu wa KUPPET kwenye kaunti ya Elgeyo Marakwet.