SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YATIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA USAID.
Serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi imenufaika pakubwa kutokana na mfumo wa ugatuzi ambao umepelekea kuafikiwa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo haikuwepo awali.
Akizungumza wakati wa kutiwa mkataba wa ushirikiano na shirika la USAID, gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amesema kuwa mfumo wa ugatuzi umepelekea ujio wa wahisani mbali mbali ambao wamechangia pakubwa kuimarika kaunti hii kimaendeleo.
Lonyangapuo ameliongeza shirika hilo kwa kuwa mshirika mkuu katika Nyanja mbali mbali hasa katika nyakati ngumu ambazo zililetwa na janga la corona kwa kuwa masitari wa mbele kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi ya corona.
Mkurugenzi wa shirika hilo nchini kenya na kanda ya afrika mashariki kwa jumla Marka Andrew meassick amesema kuwa wananuia kufanya kaunti hii mshirika sawa na USAID ili kutoa fursa kwa wakazi wa kaunti hii kunufaika na miradi ya maendeleo ambayo wamekosa kwa kipindi kirefu.