VIONGOZI MBALI MBALI WAENDELEA KUSHUTUMU MAUAJI ENEO LA KAINUK.
Aliyekuwa Waziri wa Mafuta John Munyes amelalamikia mauaji ya zaidi ya watu kumi eneo la kainuk mipakani pa Kaunti za Pokot Magharibi na Turkana.
Kwenye kikao na wanahabari mjini Kitale katika Kaunti ya Trans Nzoia, Munyes amesikitishwa na visa vya watu kuuliwa suala ambalo anahisi kwamba linaweza kusuluhishwa kupitia mikutano ya usalama baina ya jamii zinazoishi katika kaunti hizo mbili.
Kadhalika amesema maafisa wa utawala wakiwamo viongozi wa kisiasa wana jukumu kubwa kuutokomeza ihalifu huo.
Amemwomba Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai kubadilisha wakuu wa usalama wa vitengo mbalimbali hasa wakati huu taifa linapoelekea uchaguzi mkuu.