VIONGOZI WA KISIASA BONDE LA KERIO WATAKIWA KUCHUNGA NDIMI ZAO.
Jamii za kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet zimetakiwa kuishi kwa amani na kujitenga na visa vianvyosababisha utovu wa usalama hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Ni wito ambao umetolewa na viongozi bonde la kerio wakiongozwa na mwakilishi wadi maalum kaunti hii Elijah Kasheusheu na seneta wa kaunti ya Elgeyo marakwet Kipchumba Murkomen ambao aidha wamewataka viongozi wa siasa kutoka kaunti hizi mbili kuwa waangalifu na kauli ambazo wanatoa ili kuzuia hali ambayo huenda ikasababisha taharuki.
Aidha viongozi hao wameshutumu vikali madai ya Murkomen kuhusishwa na matamshi ya uchochezi, madai ambayo yanadaiwa kutolewa a kiongozi mmoja kutoka kaunti hii hali wanayosema kuwa huenda ikaleta migawanyiko kati ya jamii za pokot na marakwet.
Wamezitaka idara za uchunguzi kumakinika katika majukumu yao na kuhakikisha kiongozi yeyote anayetoa matamshi ya uchochezi anakabiliwa kisheria.