VIJANA WAONYWA DHIDI YA KUJIHUSISHA NA DHULUMA ZA JINSIA TRANS NZOIA.


Jaji wa mahakama ya Rufaa mjini Kisumu Patrick Kiage amesikitikia idadi kubwa ya kesi za dhuluma za kimapenzi zinazoripotiwa kila siku katika nyingi ya mahakama za humu nchini ikihusisha vijana wa kiume.
Akihutubu eneo bunge la Cherangani Kaunti ya Trans Nzoia, Kiage amewaonya vijana dhidi ya kujihusisha na dhuluma hizo akisema sheria haitasita kuchukua mkondo wake kwa watakao patikana na kosa hilo.
Ameongeza kwamba mhusika anaweza hukumiwa hata maisha gerezani, akionya vijana dhidi ya kujihusisha na ngono ya mapema akisema huenda ikawaharibia maisha yao ya usoni na badala yake kutaka vijana kutilia maanani masomo yao.