MBUZI AINA YA GALA WAENDELEA KUTOLEWA KWA WAKULIMA POKOT MAGHARIBI.
Wafugaji katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutunza vyema mifugo ambao wamepewa na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ili kuimarisha kilimo chao cha ufugaji.
Akizungumza baada ya kutolewa mbuzi alfu 1,095 aina ya gala ambao wanatarajiwa kupewa wafugaji kutoka wadi za Alale, Endough, Sook, Seker na Lomut, mshirikishi wa mradi wa kilimo wa Kenya climate smart Philip Ting’aa amesema hadi kufikia sasa takriban mbuzi alfu 3 na kondoo 800 wametolewa kwa wafugaji maeneo hayo.
Aidha Ting’aa amesema tayari mbuzi hao wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa CCBP huku akitoa wito kwa wafugaji kuhakikisha kuwa wanawapeleka mifugo yao maeneo kunakotolewa chanjo hiyo ili kuhakikisha usalama a mifugo yao pindi itakapotangazwa.