VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA KATIKA MAKUNDI NA KUSAJILI KAMPUNI ZAO TRANS NZOIA.
Wito umetolewa kwa vijana waliohitimu kwenye vyuo vya anuwai Kaunti ya Trans-Nzoia kujiunga katika makundi na kusajili Kampuni ili kufaidi asilimia 5% ya kandarasi kutoka kwa serikali.
Akihutubu kwenye hafla ya kutoa msaada wa vifaa vya kiufundi kwa zaidi ya vijana 132 kupitia kwa ufadhili wa child Rescue Kenya, kiongozi wa vijana katika kaunti ya Trans nzoia John Sifuna Matala ametaka vijana wenye umri wa miaka 35 kurudi chini kuchukua cheti cha AGPO kitakachowawezesha kufaidi tenda hizo.
Wakati huo huo Matala ambaye ametangaza nia ya kugombea kiti cha mwakilishi wadi ya Kapomboi amesema kuwa atashinikiza utekelezwaji wa asilimia 5 ya tenda ambazo zimetengewa vijana pamoja na kuhakikisha asilimia 95 ya ajira kwa vijana.
Aidha amewahimiza vijana kutumia teknolojia ya sasa ya utandawazi katika mauzo ya bidhaa watakayo tengeneza mbali na kupata ufahamu wa masoko kwa bidhaa zao za Kiufundi.