MBUNGE WA POKOT KUSINI ASHUTUMIWA KWA KUJIPIGIA KIFUA MIRADI YA SERIKALI.
Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kumkosoa mbunge wa Pokot kusini David Pkosing kufuatia madai yake kuwa baadhi ya miradi ya ujenzi wa barabara katika kaunti hii imetekelezwa kufuatia juhudi zake kama mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu barabara.
Wa hivi punde kuzungumzia hilo ni waziri wa utalii, utamaduni, vijana, maswala ya jinsia na huduma kwa jamii Joel Arumonyang amedai kuwa Pkosing anajipiga kifua kwa miradi iliyoratibiwa na serikali kuu hata kabla yake kuwa mbunge.
Aidha Arumonyang ambaye ametangaza nia ya kugombea kiti cha ubunge eneo la Pokot Kusini amedai licha ya Pkosing kujipiga kifua kuhusu barabara ambazo amejenga kaunti hii, wakazi maeneo mengi ya Pokot kusini wanakabiliwa na wakati mgumu kusafiri kufuatia ubovu wa barabara eneo hilo.