VIONGOZI KAUNTI YA TRANSNZOIA WAMSUTA VIKALI KATIBU MKUU WA MUUNGANO WA VYAMA VYA WAFANYIKAZI NCHINI COTU


Na Benson Aswani

Baadhi ya viongozi kutoka eneo la magharibi ya nchi wamemsuta vikali katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini cotu francis atwoli kwa madai ya kuwadhalilisha viongozi wa eneo hilo.
Wakiongozwa na mbunge wa kabuchai majimbo kalasinga na mwenzake wa kwanza ferdinand wanyonyi wamemshutumu atwoli kwa kuonekana kumdunisha kinara wa ford kenya moses wetangula pamoja na musalia mudavadi.
Viongozi hao wamemtaka atwoli kukoma kuwavuruga viongozi wa eneo hilo kwa kuwaponda bila sababu zozote huku wakimtaka kushughulikia changamoto zinazowakumba wafanyakazi na kujiepusha na siasa.