UONGOZI WA GAVANA LONYANGAPUO WAENDELEA KUKOSOLEWA.


Viongozi mbali mbali wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kukosoa uongozi wa gavana John Lonyangapuo kwa kile wamedai amefeli kutekeleza maswala yenye umuhimu mkubwa kwa wakazi wa kaunti hii.
Wakiongozwa na mgombea kiti cha ubunge eneo la Kacheliba John Lodinyo, wanasiasa hao wamesema kuwa idara muhimu hasa ile ya afya zimeendelea kudorora kutokana na huduma duni ambazo zinatolewa katika idara hiyo hali anayoihusisha na uongozi mbaya.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mgombea kiti cha eneo bunge la Pokot kusini Stephen Kolemuk ambaye ametaka ukaguzi kufanywa kwa viongozi kaunti hii kubaini walikotoa mali wanazomiliki huku akidai huenda wanatumia fedha za umma kuendeleza shughuli zao za binafsi huku wananchi wakikosa huduma muhimu za afya.