MAAFISA WA KUKUSANYA USHURU WALAUMIWA KWA KUTUMIA NGUVU MAKUTANO.

Na Benson Aswani

Maafisa wa kukusanya ushuru mjini makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelaumiwa vikali kutokana na jinsi wanavyotekeleza majukumu yao ya kukusanya ushuru hasa kutoka kwa wahudumu wa boda boda ambapo imedaiwa wanatumia nguvu kupita kiasi.
Baadhi ya viongozi kutoka katika kaunti hii ya Pokot magharibi wakiongozwa na mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu wamesema kuwa japo ni jukumu la wahudumu hao kulipia ushuru, maafisa hao hawana ruhusa ya kutumia nguvu kukusanya ushuru hasa wakati huu ambapo uchumi umeathirika pakubwa.
Kasheusheu sasa anatoa wito kwa wizara husika kuleta nidhamu katika idara ya kukusanya ushuru, kuwapa maafisa hao sare rasmi, vitambulisho vya kazi pamoja na kuhakikisha wanapata mafunzo ya jinsi ya kutekeleza majukumu yao.