WANAKANDARASI WAHIMIZWA KUWATUMIA VIJANA WA ENEO LA POKOT KWA KUWAPA KAZI


Wanakandarasi na wasimamizi wa shughuli ya ujenzi wa barabara eneo bunge la Kapenguria katika kaunti hii ya pokot magharibi wametakiwa kuhakikisha kuwa wakazi wa eneo bunge hili ndio watatumika katika shughuli hiyo.
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema kuwa kamwe hatokubali watu kutolewa maeneo mengine kujenga barabara hizo isipokuwa wataalam wa uhandisi kutekeleza shughuli ambazo zinahitaji utaalam wao.
Wakati uo huo Moroto amewataka wanakandarasi hao kuhakikisha wanafanya kazi ya kuridhisha akiongeza kuwa atalazimika kufanya doria kukagua barabara kadhaa ambazo zinajengwa ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika inaafikia viwango hitajika.