WENYEJI WANAOISHI MIPAKANI WAHIMIZWA KULETA MAENDELEO ENEO LA SUGUTA BAADA YA AMANI KUREJEA


Naibu kamishina wa Turkana mashariki katika kaunti ya Turkana Said shaaban ametoa wito kwa serikali za kaunti hii ya Pokot magharibi, Turkana na Baringo kuweka mikakati ya kuleta miradi ya maendeleo katika bonde la suguta.
Shaaban amesema kuwa tayari amani imerejea katika eneo hilo ambalo limekuwa uwanja wa mapigano ya jamii za wafugaji kwa muda mrefu, na sasa ipo haja ya wakazi kupewa maendeleo.
Shaaban amesema kuwa mizozo katika eneo hilo hasa kati ya jamii ya pokot na turkana ilikuwa ikichochewa na ukosefu wa miundo msingi ikiwemo shule hospitali na barabara, ila juhudi za wazee kutoka jamii zote mbili zimefanikiwa kuleta utulivu maeneo haya.