CHANJO YA KUZUIA KICHAA CHA MBWA YAZINDULIWA POKOT MAGHARIBI.
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi walio na mbwa pamoja na paka wametakiwa kuwaleta ili wapokee chanjo dhidi ya ugoinjwa wa kichaa cha mbwa.
Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo eneo la murkwijit eneo bunge la Kapenguria, mkurugenzi wa afya ya umma katika kaunti hii Richard Kakure amesema zoezi hilo litaendelezwa kaunti nzima ili kuhakikisha kuwa wanazuia uwezekano wa kutokea ugonjwa huo hatari baada ya kuumwa na mbwa.
Aidha kakure amesema kuwa kutaandaliwa mafunzo kwa umma kuhusu ugonjwa wa kichaa cha mbwa ili kuwawezesha wakazi na wamiliki wa wanyama hao kuwa na ufahamu kuhusu hatari ya ugonjwa huo na kuona haja ya kuhakikisha wanachanjwa kwa wanaowamiliki.