VIONGOZI WATAKIWA KUIMARISHA MIUNDO MSINGI ALALE POKOT MAGHARIBI.
Viongozi eneo bunge la kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuangazia kikamilifu changamoto ambazo zinawakumba wakazi hasa katika eneo la Akoret wadi ya alale.
Wakiongozwa na Emmanuel Napareng wakazi hao wamesema kuwa wanapitia wakati mgumu kufikia huduma muhimu kutokana na ubovu wa barabara za eneo hilo wakitoa wito kwa mwakilishi wadi wa eneo hilo kuangazia swala hilo.
Aidha wametaka kuimarishwa viwango vya elimu eneo hilo kupitia kujengwa shule zaidi wakilalama kuwa shule moja iliyokuwepo haihudumu tena baada ya mfadhili aliyekuwa akiishikilia aliuondoa ufadhili wake.