MARUFUKU YA SIASA MAKANISANI YAENDELEA KUIBUA HISIA.
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia hatua ya baadhi ya makanisa kupiga marufuku viongozi wa siasa kupeleka siasa katika maabadi.
Baadhi ya wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wameunga mkono hatua hiyo wakisema kuwa kanisa ni sehemu ambayo inafaa kuheshimiwa na viongozi wote kwani ni eneo la maombi na kiongozi yeyote hastahili kupeleka maswala ya siasa kanisani.
Wamesema kuwa iwapo kiongozi yeyote wa kisiasa atataka kulisaidia kanisa kifedha basi anafaaa kufanya hivyo kwa utulivu na kuendeleza siasa nje ya maabadi baada ya kukamilika ibaada za kanisani.
Hata hivyo wapo baadhi ya wakazi ambao wametofautiana na hatua hiyo wakisema kuwa viongozi wa kisiasa wanafaa kupewa fursa ya kuhudhuria ibaada hizo na hata kuhutubia waumini.