BIDHAA ZA WIZI ZAKAMATWA KAPENGURIA.


Polisi katika kituo cha polisi cha kapenguria wamepata baadhi ya bidhaa za wizi kufuatia oparesheni ambayo inaendeshwa kuwanasa washukiwa wa misururu ya wizi ambayo imekuwa ikiripotiwa eneo la kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi.
Tayari mshukiwa mmoja wa wizi ametiwa mbaroni na anazuiliwa ili kusaidia katika kuwatafuta washukiwa wengine.
Silas teketeke mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa bendera alikamatwa mapema jana kufuatia ushirikiano baina ya wakazi wa eneo hilo na maafisa wa polisi baada ya kubomoa duka moja eneo hilo na kuiba simu pamoja na mitungi ya gesi, na kisha kuiba shilingi 200 kutoka duka la dawa la kape chem eneo lilo hilo.
Inadaiwa mshukiwa ni mmoja wa wahalifu ambao wamekuwa wakiendeleza misururu ya wizi ambapo mwezi mei anadaiwa kuiba shilingi alfu 106 pamoja na pikipiki kutoka duka hilo la dawa la kape chem.
Ni kisa ambacho kimekashifiwa vikali na mwakilishi wadi maalum Elijah Kashesheu ambaye amewataka wakazi eneo hilo kuwa makini na kushirikiana na maafisa wa usalama kuhakikisha visa hivi vinakabiliwa.
Kasheusheu ametoa wito kwa idara ya usalama kaunti hii ya Pokot magharibi ikiongozwa na kamishina Apolo Okelo kuimarisha doria hasa nyakati za usiku ambapo amesema visa vingi vya wizi hutekelezwa, na kusafirishwa bidhaa za wizi.