SERIKALI YATAKIWA KUTWAA SILAHA ZINAZOMILIKIWA KINYUME CHA SHERIA KERIO VALLEY.


Wito umetolewa kwa serikali kuendesha oparesheni ya kuondoa silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria miongoni mwa raia katika bonde la Kerio hasa eneo la Chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet.
Mkurugenzi wa amani katika kaunti hii ya Pokot magharibi Joel Limakina amesema kuwa juhudi za kuhakikisha amani inaafikiwa eneo hilo hazitaafikia lolote iwapo baadhi ya wakazi watakuwa wangali wanamiliki silaha kinyume cha sheria.
Wakati uo huo Limakina ametoa wito kwa wadau ikiwemo wazee kutoka pande zote mbili pamoja na mashirika ya kibinadam kushirikiana na serikali katika kuhakikisha utovu wa usalama ambao umeshuhudiwa eneo hilo kwa muda mrefu unapata suluhu.