WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MVUA INAYOSHUHUDIWA KUPANDA MIMEA YA CHAKULA.
Wito umetolewa kwa wakulima katika kaunti hii ya pokot magharibi kutumia mvua inayoshuhudiwa maeneo mbali mbali ya kaunti hii kuendeleza kilimo cha mimea mbali mbali hasa baada ya kuathirika mahindi kufuatia kuchelewa mvua mapema mwaka huu.
Ni wito wake afisa mkuu katika wizara ya kilimo kaunti hii Samson Nyang’aluk ambaye aidha amesema kuwa serikali ya kaunti inaendelea kukamilisha mradi wa ununyiziaji maji mashamba ili kukabili tatizo la ukame ambao husababisha baa la njaa kaunti hii.
Wakati uo huo Nyang’aluk ameyapongeza mashirika yasiyo ya serikali ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali ya kaunti kupitia wizara ya kilimo kwa kuendeleza miradi ya kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula kwa wenyeji huku akitoa wito kwa mashirika zaidi kujitokeza kuchangia juhudi hizo.