VISA VYA WAKAZI KUUMWA NA NYOKA VYAKITHIRI LOMUT.


Wakazi wa eneo la Lomut katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia ongezeko la visa vya wakazi kuumwa na nyoka eneo hilo.
Wakiongozwa na aliyekuwa diwani wa Lomut Musa Tekelezi wakazi hao wamesema kuwa huenda hali hii imechangiwa na ongezeko la joto ambalo linawalazimu nyoka hao kutoka maeneo yao ya maficho na kuingia katika makazi ya watu.
Ametaka maafisa kutoka idara ya wanyamapori kuzuru eneo hilo na kuangazia hali ilivyo ili kuwanusuru wakazi.
Kando na hayo Tekelezi amelalamikia hali mbovu ya barabara za eneo hilo akitaka serikali ya kaunti kuwajibikia swala hilo.