WAKAZI WA OROLWO, POKOT MAGHARIBI WALALAMIKIA UHABA WA MAJI.
Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi kupitia wizara ya maji na mazingira kuhakikisha wakazi wa orolwo wanapata maji safi kupitia uchimbaji wa visima vya maji eneo la hilo.
Wakiongozwa na Daniel Kamarkan, wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya kupata maji safi kwani kwani kwa sasa wanalazimika kutumia maji ya bwawa lililoko na ambayo si salama kwani wanayatumia pamoja na mifugo hali ambayo ni hatari kwa afya yao.
Wakati uo huo wakazi hao wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuwajengea daraja katika mto unaopatikana eneo hilo ili kurahisisha shughuli za usafiri ambao wanasema huathirika pakubwa kunaposhuhudiwa mvua kubwa ambapo hufurika na kuhatarisha usalama wao hasa wanafunzi wanapoelekea shuleni.