IDARA YA USALAMA YASUTWA KWA KUITELEKEZA POKOT MAGHARIBI KATIKA MASWALA YA USALAMA.
Idara ya usalama nchini imeshutumiwa vikali kwa kutozingatia usawa katika kuhakikisha amani inadumishwa mipakani mwa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet.
Mwakilishi wa kike katika kaunti hii ya Pokot magharibi Lilian Tomitom amedai kuwa serikali imeitelekeza pakubwa kaunti hii katika kuweka mikakati ya kuhakikisha usalama unadumishwa kinyume na ilivyo katika kaunti ya elgeyo marakwet.
Kwa upande waka mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amemshutumu inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutiambai kwa kutotelekeza majukumu yake ya kuhakikisha polisi wanawahudumia wanachi vyema na badala yake kutumika kisiasa na watu fulani serikalini.