WAKAZI WA EX-SOLONZO TRANS NZOIA WATAKA KUPEWA ARDHI MBADALA.
Wenyeji wa eneo la Gitwamba eneo bunge la Saboti Kaunti ya Trans-Nzoia wametaka wizara ya ardhi nchini kuharakisah mpango wa kuwapa ardhi mbadala baada yao kurufushwa kwenye shamba la Ex-Solonzo lenye takriban ekari 600 mnamo mwaka wa 2019 na baadaye serikali kuahidi kuwakutafutia ardhi mbadala.
Kwenye Mkao na wanahabari wenyeji hao wameelezea masaibu wanayopitia tangu kufurushwa kwao kwenye ardhi hiyo waliyotoa fedha na kununua mnamo mwaka wa 1999 wakitaka serikali iwapo imeshindwa kuwatafutia ardhi nyingine kuwaruhusu kurejea kwenye ardhi hiyo.
Kwa Upande wake mbunge wa Saboti Caleb Amisi amesema amewasilisha swala hilo katika bunge la Kitaifa akiwaahidi wenyeji kuwa swala hilo litatuliwa kabla ya hatamu yake ya kwanza ya uongozi eneo bunge hilo kukamilika,akitoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta anapotarajiwa kuzuru Kaunti ya Trans-Nzoia kushughulikia maswala yote ya ardhi Kaunti hiyo ikiwa ni pamoja na utata wa umiliki wa shamba la Mengo eneo bunge hilo.