KAUNTI YA TRANS NZOIA KUPOTEZA ASILIMIA 30 YA NAFAKA MWAKA HUU.
Huenda kaunti ya Trans nzoia ikapoteza asilimia 30 ya nafaka mwaka huu kutokana na upungufu wa mvua ambayo imeshuhudiwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Haya ni kwa mujibu wa mshauri mkuu wa kiseharia katika afisi ya naibu rais Dkt Abraham Sing’oei ambaye ametaka serikali kuweka mikakati kuhakikisha mazao kutoka kwa wakulima yananunuliwa na serikali kwa bei ya kumfaidi mkulima.
Wakati uo huo Sing’oei ameleezea haja ya serikali za kaunti kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili kuzuia kushuhudiwa upungufu wa mvua hasa katika kaunti ya Trans nzoia ambayo ni eneo la kilimo.