‘TAREHE YA UCHAGUZI HAITOBADILISHWA’ ASEMA SING’OEI.
Mshauri mkuu wa kisheria katika afisi ya naibu wa rais dkt abraham singoei, amekosoa vikali matamshi ya baadhi ya viongozi nchini ya kutaka kubadilishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 akisema ni ukiukaji mkubwa wa katiba.
Singoei ambaye pia ametangaza nia ya kugombea kiti cha ugavana kaunti ya trans-nzoia amesema hatua ya kubadili tarehe ya uchaguzi ni tishio kwa demokrasia, amani na hujuma kwa ukuaji wa uchumi wa kitaifa.
Aidha dkt Singoei amesema hatua ya kubadili tarehe ya uchaguzi kikatiba inaweza tu kufanyika iwapo kutakuwepo vita baina ya Kenya na taifa lingeni na hilo halipo kwa sasa hivyo jaribio la kubadili tarehe hiyo ya uchaguzi itakuwa kinyume cha katiba ya mwaka wa 2010.
Wakati huo huo ametaka wanaotoa matamshi ya kubadilishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu nchini kuchunguzwa na taasisi za serikali kwani huenda wana nia fiche ya kuhujumu usalama wa kitaifa.