UCHACHE WA MVUA WATISHIA USALAMA WA CHAKULA POKOT MAGHARIBI


Wito umetolewa kwa serikali ya kitaifa kupitia wizara ya ugatuzi kuweka mikakati ya kuwasaidia wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi kwa kuleta msaada wa chakula kufuatia tishio la kushuhudiwa baa la njaa.
Akizungumza na kituo hiki aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hii ya pokot magharibi katika serikali iliyotangulia simon kalekem, amesema kuwa uhaba wa mvua ambao umeshuhudiwa katika kaunti hii umepelekea mimea ya wakulima wengi kunyaukia shambani ambapo sasa wakulima hawatarajii mavuno yoyote mwaka huu.
Aidha Kalekem ameitaka serikali ta kaunti hii ya Pokot magharibi ikiongozwa na gavana John Lonyangapuo kusitisha baadhi ya miradi inayoendeleza na badala yake kutumia fedha hizo kununua chakula ambacho kitawafaa wakazi wa kaunti hii watakaokabiliwa na njaa.
Wakati uo huo Kalekem ameshutumu idara ya majanga katika kaunti hii kwa kile amedai kutowajibika katika majukumu yake huku akitaka afisi ya gavana kuchukua majukumu yote ambayo yalikabidhiwa idara hiyo aliyoitaja kuwa isiyostahili kuwepo.