‘MCHAKATO WA KUIFANYIA KATIBA MAREKEBISHO KUREJELEWA’ ASEMA SENETA WA BARINGO GIDEON MOI
Seneta wa kaunti ya Baringo Gideon Moi ameelezea imani kwamba majaji saba wa mahakama ya rufaa walioskiza kesi za kupinga kuharamishwa kwa mchakato wa BBI watabatilisha uamuzi uliotolewa na majaji wa mahakama kuu.
Akiongea kwenye eneo bunge la Mogotio seneta Moi amesema kuwa mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia mpango wa BBI utarejelewa baada ya majaji hao kutoa uamuzi wao.
Seneta Moi amesema kuwa mapendekezo yaliyo kwenye mswada wa BBI yatawafaidi zaidi wakazi wa kaunti ya Baringo na pia wakenya kwenye maeneo yote ya taifa.
Majaji saba walioskia kesi za rufaa za kupinga kuharamishwa kwa mswada wa BBI wameratibu tarehe 20 mwezi ujao wa Agosti kama siku watakapotoa uamuzi wao kuhusu kesi hiyo.