UTEUZI WA NAIBU CHIFU MPYA YUALATEKE WAPINGWA NA WAKAZI.

Wakazi wa yualateke eneo la kipkomo kaunti hii ya pokot magharibi wameandamana wakilalamikia kuteuliwa naibu chifu eneo hilo wakidai si mkazi wa eneo hilo.
Wakiongozwa na Wilson Amanang’ole wakazi hao wamedai kuwa uteuzi wa chifu huyo ulighubikwa na maswala ya ufisadi na kuingiliwa na wanasiasa ambao nia yao ni kuwaleta watu watakaowasaidia katika kampeni za uchaguzi wa mwaka ujao.
Uteuzi wa naibu chifu huyo kwa jina Japheth Ruto ulijiri baada ya kifo cha chifu Moses Loyatum mapema mwaka huu.
Wakazi hao wamesema kuwa wapo zaidi ya wakazi watano wa eneo hilo ambao walituma maombi ya kujaza nafasi hiyo ila hawakuzingatiwa huku wakiapa kuendelea kuandamana hadi uteuzi wa naibu chifu huyo utakapobatilishwa wakitaka wakuu wa idara za usalama kaunti hii kuchunguzwa.
Akizungumzia swala hilo naibu kamishina wa eneo hilo James Wambua amesema kuwa hajapata malalamishi kutoka kwa wakazi hao kwani alikuwa kwenye likizo akiwataka wakazi kuwa na utulivu swala hilo linaposhughulikiwa.