GAVANA WANGAMATI ASHUTUMIWA KWA MADAI YA KUFADHILI GHASIA MAZISHINI BUNGOMA.
Gavana a kaunti ya Bungoma Wyclife Wangamati ameshutumiwa kwa madai ya kutumia maafisa wa serikali yake kusababisha ghasia hasa katika hafla za mazishi.
Kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hiyo Joseph Juma amedai kuwa gavana Wangamati anawashinikiza maafisa wa serikali yake kumtengea fedha za kufadhili ghasia hizo.
Juma anadai kuwa amepokea ushahidi kutoka kwa baadhi ya maafisa hao ambao hushinikizwa kutoa fedha hizo ambazo wanasema huzitoa kwa hofu.