WAFANYIKAZI WA UMMA WASHINIKIZA KUPEWA NYONGEZA YA MSHAHARA LICHA YA SRC KUSEMA HAITAWAONGEZA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI


Tume ya kutathmini mishahara ya wafanyakazi SRC inaendelea kushutumiwa kutokana na msimamo wake kwamba wafanyakazi wa umma hawataongezewa mishahara katika kipindi cha miaka miwili.
Akiongea mjini Kakamega mwenyekiti wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo anwai KUPPET Johnson Wabuti ameikosoa tume hiyo kwa kukiuka mkataka wa awali ulioafikiwa baina ya serikali na chama hicho.
Wabuti amesema kuwa licha ya uchumi wa taifa kuathirika kwa kiwango flani kutokana na janga la virusi vya korona walimu wanastahili kuongezewa mshahara kwani gharama ya maisha inaendelea kupanda.
Wabuti aidha ameongeza kuwa serikali haipaswi kuwanyima nyongeza ya mshahara ilhali imeshindwa kukabili janga la ufisadi ambalo hupelekea taifa kupoteza mabilioni ya pesa kila mwaka.