WANASIASA TRANS NZOIA WAONYWA DHIDI YA KUENDELEZA SIASA ZA CHUKI.


Uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 unapokaribia, wito umetolewa kwa wanasiasa katika kaunti ya Trans nzoia kuendeleza siasa za amani na kutosababisha kupanda joto la siasa nchini.
Aliyekuwa seneta wa kaunti hiyo Henry ole Ndiema amesema kuwa ni wakati wanasiasa wote wanaolenga kuwania nyadhifa za siasa kuuza sera zao kwa wananchi kwa njia ya utulivu bila kusababisha hali ambayo huenda ikapelekea chuki za kikabila kaunti hiyo.
Ole Ndiema amewataka wanasiasa wote kufahamu kuwa wananchi wanafahamu kiongozi bora watakayemchagua na kuwa sera zao ndizo zitakazoamua hatima yao wala hawatochaguliwa kwa misingi ya kuwaharibia wenzao majina.