PUKOSE ATOA MATIBABU YA BURE YA UPASUAJI KWA WENYEJI WA ENDEBES
Mbunge wa Endebess DKT Robert Pukose aliadhimisha siku ya madaraka kwa kutoa huduma bure za afya kwa wenyeji wa eneo bunge lake ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kutokana na gharama ya juu ya matibabu ya upasuaji.
Kwenye mkao na wanahabari baada ya kufanya upasuaji kwa wagonjwa watano katika hospitali ya kaunti ndogo ya Endebess, Dkt Pukose ameelezea kuwa amechukua hatua ya kusherehekea madaraka kwa kugusa maisha ya mwananchi wa kawaidi ambaye anapitia wakati mgumu kufuatia kupanda gharama ya utoaji wa huduma za afya nchini.
Kwa upande wake Dkt Simon Kapchanga ambaye pia ni mwenyeji wa eneo bunge hilo ametoa wito kwa wenyeji eneo hilo kujisajili kwa bima ya afya ya nhif ili kusaidia kumpunguzia mgonjwa gharama ya matibabu haswa ya upasuaji.