WADAU WA USALAMA WATAKIWA KUIMARISHA VITA DHIDI YA MIMBA ZA MAPEMA TRANS NZOIA.
Zaidi ya wanafunzi alfu 1, 120 katika kaunti ya Trans nzoia wamepachikwa mimba tangu kuripotiwa nchini kisa cha kwanza cha virusi vya corona tarehe 15 mwezi machi mwaka jana.
Haya ni kulingana na kamishina wa kaunti hiyo Sam Ojwang ambaye amesema kuwa wanashirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo viongozi wa dini na wazee wa mitaa katika kuhakikisha kuwa visa hivyo vinakabiliwa katika kaunti ya trans nzoia.
Akithibitisha kukamatwa zaidi ya washukiwa 50 wa visa hivyo, Ojwang aidha amekariri onyo la serikali kuwa maafisa wa serikali katika maeneo ambako kutashuhudiwa kisa cha mwanafunzi kupachikwa mimba atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufutwa kazi.